JINA LAKO LITUKUZWE #MATHAYO 6:9
JINA LAKO LITUKUZWE #MATHAYO 6:9 MPENDWA WANGU NIMEKUKUMBUSHA SEHEMU YA KILE TULICHOANDIKA KATIKA KITABU CHAKO CHA ‘KUWA NA UJUZI KATIKA MAOMBI’ UKURASA WA 14. HEBU JIFUNZE KITU KATIKA SEHEMU HII. -------------------------------- Mwana wa Mungu, Jina la kiumbe chochote kile duniani huwa lina akisi tabia ya kiumbe hicho. Nadhani wajua hata wewe unapenda uitwe kwa jina lako maana ndani ya jina lako limekubeba wewe mwenyewe. Majina huwa yanabeba tabia zetu. Majina huwa yana akisi tabia zetu. Ndiyo maana wazazi wanashauriwa sana kuwa makini wanapowapa majina watoto wao. Ni lazima yaakisi maana halisi ya kile wanachotaka kukimaanisha. Sio vizuri kumpa mtoto jina ili mradi ni jina kwa sababu jina hilo hubeba tabia ya huyo mtoto. Wajua tena mara nyingi tu watu wengi unawaona mtaani tabia zao zinalingana kabisa na majina yao. Kwa nini? Kwa sababu nyakati zingine majina hayo hubeba roho zikisimamia tabia za majina hayo. Usimpe mtoto tu kwa sababu ni jina. Ndivyo ilivyo mwa...