TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA.

TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA.

Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;  akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;  ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,  Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa,  Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia. TOKEA WAKATI HUO YESU ALIANZA KUHUBIRI, NA KUSEMA, TUBUNI; KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA. #MATHAYO 4:12-17

Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu.
Kwanza nikutakie ibada njema mpendwa wangu ambaye leo ni siku yako ya ibada.

Kila siku ya jumapili huwa siachi kuzungumza jambo kwa ajili ya kanisa kuboresha ibada zetu.  Yamkini Neno hili katika #Mathayo 4:17 likawa si neno lenye kuhubiriwa kwa sauti kubwa na yenye nguvu katika baadhi ya madhehebu mengi lakini acha niseme jambo leo kuhusu toba kama msingi wa Injili ya kweli ya Kristo.

Neno la Mungu linasema kwamba ‘Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO’ #WAEBRANIA 12:14. Ni muhimu sana tujue msingi huu kwamba pasipo utakatifu hakuna mbingu mwanadamu ataiingia.  Na kama ndivyo lazima Injili zetu sisi watumishi wa Mungu zijikite katika watu kufikia toba ya kweli. Lazima ifike mahali kila muumini alitambue hili. Na kila mtumishi wa Mungu unapaswa kusima kidete pasipo kupepesa macho kukemea dhambi katikati ya kondoo pasipo kujali kondoo hataleta chakula tena hekaluni kisa umemkanya. Sasa kuna maeneo mengine unapogusa eneo la toba kwa kweli inakuwa shida. Lakini niseme hivi Toba ndio msingi wa injili.

Tangu mwanadamu apotee pale bustani ya Edeni Mungu amekuwa na kazi moja tu ‘kumrejesha mwanadamu katika mahusiano naye Mungu’. Hivyo manabii walioibuka walijenga kwa msingi ambao Kristo atakuja kuusimamia nao ni toba ya kweli itokayo mioyoni mwa watu. Ndiyo maana Kristo alivyokuja alijenga msingi wa Injili yake katika toba ili watu wamrudie Mungu. Ni kuwafanya watu watubu na kumrudia Mungu, wabadilishe fahamu zao na mienendo yao na wawe viumbe vipya. Mambo mengine yalifuata lakini msingi wa kwanza ni Toba. Uponyaji wa kimwili, kuwafungua watu mapepo, utajiri na mengineyo ambayo ni mema kabisa katika utauwa vilifuata, lakini kwanza ilikuwa toba.

Manabii walitangulia kuweka msingi wa Injili kwamba ni Toba. Nabii Isaya asema: "Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake" #ISAYA 40:3
Yohana Mbatizaji kama mtangulizi wa Kristo alisimamia katika msingi huo. Asema "Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia" - #MATHAYO 3:2

Nimegundua wakati mwingine hata kufunguliwa kwa mtu kumekuwa rahisi sana ukianza na toba. Na maandiko yanasema ‘Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa’.

Waweza kuzunguka kushoto na kulia, mbele na nyuma lakini katika kuhubiri kwetu Injili msingi wake utabaki kuwa toba ya kweli inayobadilisha ufahamu wa mwanadamu na kumfanya kuwa kiumbe kipya.

Bwana Yesu asema hata damu yake iliyomwagika pale msalabani ilikuwa ni kwa ajili ya kuwaondolea wanadamu dhambi zao.

Malaika alivyoenda kwa Yusufu kwenda kumtangazia habari njema za kuzaliwa kwa mwokozi Yesu kupitia kwa mchumba wake Mariamu msingi wa tangazo hilo ulisimama katika toba.
"Usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, YEYE NDIYE ATAKAYEWAOKOA WATU WAKE NA DHAMBI ZAO" - #MATHAYO 1:20,21
Na hata Bwana Yesu mwenyewe akasema "kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi KWA ONDOLEO LA DHAMBI" - #MATHAYO 26:28

Wakati Wayahudi na watu wengine wakishaangaa siku ile ya Pentekoste, Petro alisimama na kuwaambia "TUBUNI mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu" #MATENDO 3:38
Kumbe hatuwezi kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kama hatujakubali kutubu na kumrudia Mungu.

“Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa ANAWAAGIZA WATU WOTE WA KILA MAHALI WATUBU.  Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu” #MATENDO 17:30-31

Kwa hiyo kutubu ni agizo linalotukaribisha katika utakatifu na kuwa na mahusiano na Mungu wa kweli. Mungu anaagiza watu wote watubu. Nami nakuagiza katika jina la Yesu utubu ndugu yangu. Katika eneo lolote ambalo halijakaa vizuri na Mungu wako nakuagiza tubu na utakaswe kwa damu ya Yesu. Hakuna mwenye dhambi atakayeingia mbinguni #1KOR. 6:9

Mungu akubariki.

Share ujumbe huu na mtu mwingine naye abarikiwe.

YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU, KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA ‪#‎MARKO‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬ 10:27‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬

Kwa maombi na maombezi, unataka kupokea uponyaji au kufunguliwa kwenye kifungo chochote kile, ushauri au unatamani ujitoe kikamilifu kumtumikia Mungu na UNATAKA KUMPOKEA BWANA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO NA AKUSAMEHE DHAMBI ABADILISHE MAISHA YAKO NA TABIA MBAYA ZILIZOKUSHINDA basi tupigie au tutumie ujumbe kwa namba +255 758 443 873 au 0713 783 565

KWA MIJINI NA VIJIJINI JE MNA UHITAJI WA SEMINA ZA NENO LA MUNGU AU MIKUTANO YA INJILI? WASILIANA NASI KWA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU TUJE TUFANYE HUDUMA HUKO. TUMEAMRIWA ‘ENENDENI ULIMWENGUNI MWOTE, MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE’ #MARKO 16:15.

NA MUNGU AMEKWISHA KUACHILIA NGUVU KUU JUU YA KANISA ITUMIKE KUFUNGUA WATU KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA KWENYE NDOA, BIASHARA, KAZI, NA MAISHA KWA UJUMLA. YEYE MWENYEWE AMESEMA ‘NITALIJENGA KANISA LANGU WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA’. IKO NGUVU JUU YA KANISA NDUGU. BWANA YESU ANATUAGIZA ‘NA KATIKA KUENENDA KWENU, HUBIRINI, MKISEMA, UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA. POZENI WAGONJWA, FUFUENI WAFU, TAKASENI WENYE UKOMA, TOENI PEPO; MMEPATA BURE, TOENI BURE’ #MATHAYO 10:7-8

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINA LAKO LITUKUZWE #MATHAYO 6:9