JINA LAKO LITUKUZWE #MATHAYO 6:9

JINA LAKO LITUKUZWE #MATHAYO 6:9

MPENDWA WANGU NIMEKUKUMBUSHA SEHEMU YA KILE TULICHOANDIKA KATIKA KITABU CHAKO CHA ‘KUWA NA UJUZI KATIKA MAOMBI’ UKURASA WA 14. HEBU JIFUNZE KITU KATIKA SEHEMU HII.
--------------------------------

Mwana wa Mungu, Jina la kiumbe chochote kile duniani huwa lina akisi tabia ya kiumbe hicho. Nadhani wajua hata wewe unapenda uitwe kwa jina lako maana ndani ya jina lako limekubeba wewe mwenyewe. Majina huwa yanabeba tabia zetu. Majina huwa yana akisi tabia zetu. Ndiyo  maana wazazi wanashauriwa sana kuwa makini wanapowapa majina watoto wao. Ni lazima yaakisi maana halisi ya kile wanachotaka kukimaanisha. Sio vizuri kumpa mtoto jina ili mradi ni jina kwa sababu jina hilo hubeba tabia ya huyo mtoto.

Wajua tena mara nyingi tu watu wengi unawaona mtaani tabia zao zinalingana kabisa na majina yao. Kwa nini? Kwa sababu nyakati zingine majina hayo hubeba roho zikisimamia tabia za majina hayo. Usimpe mtoto tu kwa sababu ni jina.

Ndivyo ilivyo mwana wa Mungu katika majina ya Mungu ambayo yeye mwenyewe amejitanabaisha kwetu au yale ambayo Mitume na Manabii waliamua kumuita Mungu kwa sababu mbalimbali; siku zote majina haya yanaakisi tabia za Mungu. Ndiyo  maana mara nyingi Mungu alikuwa akibadili majina ya watu anapokuwa amewaweka katika utumishi wake ili yalingane na huduma ambayo wanaenda kukabiliana nazo. Abram alibadilishwa jina kuwa Ibrahimu, Yakobo alibadilishwa jina kuwa Israel, Saulo alibadilishwa jina na kuitwa Paulo n.k n.k. ili waweze kubeba ile huduma iliyokuwa mbele yako.

Mfano wa majina hayo ya Mungu ni kama:
i. Adonai ‐ Mungu Mwenye enzi yote ‐ Mwa 15:2‐8, Kut 6:2‐3
ii. El‐Ohim ‐ Mungu Muumbaji ‐ Mwa 33:20, Kol 1:16‐17
iii. El‐Roi ‐ Mungu Aonaye kila kitu ‐ Mith 15:3, Zab 32:8
iv. El‐Shaddai ‐ Mungu Mtoshelezi ‐ Mdo 17:28, Kumb 8:4
v. Jehovah ‐ Ajitegemeaye kuwepo ‐Kut 6:2‐8, Mdo 17:24‐25
vi. Jehovah Shalom ‐Mungu Amani yetu ‐ Amu 6:22‐24
vii. Jehovah Rapha ‐ Mungu Atuponyaye ‐ Kut 15:26
viii. Jehovah Jireh ‐ Mungu Mtoaji wetu ‐ Mwa 22: 8, 14
ix. Jehovah Nissi ‐ Mungu Ushindi wetu ‐ Kut 14:13‐14
x. Jehovah Shammah ‐ Bwana ni Aliyepo ‐ Kut 3:14
xi. Jehovah Rohi ‐ Bwana ni Mchungaji wangu ‐ Zab 23:1

Unapoingia katika maombi na kuyataja majina mbali mbali ya Mungu yanakuhuisha utu wako wa ndani, kumtukuza Mungu na kuakisi kile ambacho Mungu anakupitisha katika maisha yako au katika hali yako.

Imeandikwa ‘Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake’ #ZABURI 100:4. Kwa hiyo lazima ulisifu na kulitukuza jina la Mungu aliye hai katika maombi yako. Ndiyo moja ya njia nzuri ya kumsifu Mungu na kumtukuza. Sio wote tumepewa karama ya kuimba, lakini kwa kutumia maombi unaweza ukamsifu Mungu na moyo wako ukapata burudiko kuu maishani mwako.

Unapopita katika hali ya kuugua na kugundua Mungu ni mponyaji, utaingia katika maombi na kumwambia najua wewe ni Mungu uponyaye yaani Yehova Rapha, Mungu utuponyae na magonjwa yetu yote. Yehova Rapha nakusihi uniponye katika jina la Yesu.

Unapopita katika mapito mazito hadi imani yako inatindikiwa ni wakati mzuri kuingia kwenye maombi na kumwambia Bwana wewe ndiye Mchungaji wangu na sitapungukiwa na kitu. Hata nijapopita kwenye bonde la uvuli wa mauti Bwana wewe ni Mchungaji wangu. Nichunge hata katika mapito haya nayopitia sasa. Na ni wakati mzuri pia wa  kumwambia Bwana wewe ni Jehova Nissi yaani wewe ni ushindi wangu. Nishindie katika mapito haya nayopitia Bwana. Yako mapito mengine ni magumu na ni mazito kama huna Mungu huwezi kuyapita. Kuna mapito magumu kwenye ndoa, kazi, jamii, huduma, familia bila Jehova Nissi huwezi kushinda. Mwambie akushindie sasa.

Unapokuwa umepungukiwa na amani kwenye ndoa au familia au kazi au huduma yako mwambie Bwana wewe ndiye Jehova Shalom, Bwana wa amani iponye na kuifunika ndoa yangu na amani yako.

Unapokuwa umepungukiwa na chochote ni wakati mzuri wa kuingia kwenye maombi na kumwambia Bwana wewe ni Jehova Yire yaani Bwana we ndiye mpaji wangu.

Unapomtaja Mungu kwenye maombi kwa majina yake namna hii, utu wako wa ndani unahuishwa na Roho Mtakatifu atabadili utu wako wa ndani na kukabiliana na hali halisi unayoipitia. Kwa hiyo jifunze majina na maana mbali mbali za majina ya Mungu na yatumie katika maombi yako uone namna gani utu wako wa ndani utahuishwa. Jifunze uone.

Tambua pia Mungu amejifunua kwetu wanadamu kwa jina kuu lilipitalo majina yote jina la YESU KRISTO. 

     ...…………..
Na kitabu hili bado kipo kwa yeyote anayekihitaji na anayetamani kuinua huduma yake ya maombi

Mungu wangu aliye hai akubariki

Share ujumbe huu na mtu mwingine naye abarikiwe.
YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU, KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA ‪#‎MARKO‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬ 10:27‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬

Kwa maombi na maombezi, unataka kupokea uponyaji au kufunguliwa kwenye kifungo chochote kile, ushauri au unatamani ujitoe kikamilifu kumtumikia Mungu na UNATAKA KUMPOKEA BWANA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO NA AKUSAMEHE DHAMBI ABADILISHE MAISHA YAKO NA TABIA MBAYA ZILIZOKUSHINDA basi tupigie au tutumie ujumbe kwa namba +255 758 443 873 au 0713 783 565

KWA MIJINI NA VIJIJINI JE MNA UHITAJI WA SEMINA ZA NENO LA MUNGU AU MIKUTANO YA INJILI? WASILIANA NASI KWA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU TUJE TUFANYE HUDUMA HUKO. TUMEAMRIWA ‘ENENDENI ULIMWENGUNI MWOTE, MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE’ #MARKO 16:15.

NA MUNGU AMEKWISHA KUACHILIA NGUVU KUU JUU YA KANISA ITUMIKE KUFUNGUA WATU KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA KWENYE NDOA, BIASHARA, KAZI, NA MAISHA KWA UJUMLA. YEYE MWENYEWE AMESEMA ‘NITALIJENGA KANISA LANGU WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA’. IKO NGUVU JUU YA KANISA NDUGU. BWANA YESU ANATUAGIZA ‘NA KATIKA KUENENDA KWENU, HUBIRINI, MKISEMA, UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA. POZENI WAGONJWA, FUFUENI WAFU, TAKASENI WENYE UKOMA, TOENI PEPO; MMEPATA BURE, TOENI BURE’ #MATHAYO 10:7-8

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA.