TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA.
TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA. Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia. TOKEA WAKATI HUO YESU ALIANZA KUHUBIRI, NA KUSEMA, TUBUNI; KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA. #MATHAYO 4:12-17 Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu. Kwanza nikutakie ibada njema mpendwa wangu ambaye leo ni siku yako ya ibada. Kila siku ya jumapili huwa siachi kuzungumza jambo kwa ajili ya kanisa kuboresha ibada zetu. Yamkini Neno hili katika #Mathayo 4:17 likawa si neno lenye kuhubiriwa kwa sauti kubwa na yenye nguvu katika baadhi ya madhehebu mengi lakini...
Maoni
Chapisha Maoni